THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Mwanamuziki apata kadi bima ya afya

Na Mashaka Mhando, Tanga .

MTANDAO wa kijamii wa Wana muziki na wadau wa muziki wa dansi nchini (Kavasha), wamechanga fedha zilizowezesha mwanamuziki George Gama kupata kadi ya bima ya afya.

Mtandao huo kupitia simu za mikononi imewezesha kumkatia bima ya afya kupitia Chama cha mtandao wa Wana muziki nchini ambao ni wakala wa NHIF kama kundi chini ya mwanamuziki nguli John Kitime ambaye ni kiongozi wa mtandao huo na amepewa kadi hiyo na mfuko wa bima ya afya wanaita NHIF .

Kiongozi wa kundi la mtandaoni linalojumuisha wadau wa muziki na Wanamuziki wa dansi (Kavasha) Fredy Paschal alisema wao kama kundi wameweza kuchanga fedha kiasi cha Zaidi ya sh 76,800/= zilizowezesha mwanamuziki huyo wa zamani wa bendi mbalimbali ikiwemo Twanga Pepeta, kupata kadi hiyo aliyokabidhiwa na Katibu wa Kavasha John Shekwavi aliembatana na Mwanamuziki Tabu Mambosasa ambae ni Mweka Hazina wa kundi hilo .

Alisema sababu ya wao kuchangia gharama ya kadi hiyo kuwa ni utaratibu wa kundi kusaidiana baina ya wanachama, kusaidia kuinua muziki wa dansi na kusaidi wanamuziki hapa nchini.

Paschal aka FP alisema mwanamuziki huyo ni wa kwanza kwa utaratibu huo na kwamba hivi sasa mwanamuziki wa zamani wa bendi ya UDA jazz Mikidadi Seif na mkewe watafatia baada ya kiasi kinachohitajika kuwa tayari kimeshachangwa.

"Huyu (Gama) ni mwanamuziki wa kwanza kupata bima lakini kuna maandalizi ya kadi ya Bima ya mwanamuziki wa zamani wa UDA JAZZ Ndugu Mikidadi Seif na mkewe Bi Zulfa zipo kwenye maandalizi ya awali kupitia kundi la PSPF ambavyo vyote ni michango ya wanachama wa kundi la Kavasha, "alisema Paschal.

Alisema utaratibu wa kundi hilo la Kavasha ni kuwa ni kuwasaidia mwanachama wao ingawa wamekuwa pia wakiwasaidia wanamuziki hasa wasio na misaada ikiwemo fedha za matibabu kupitia michango kwa wanamuziki kadhaa na wanachama pia pamoja na msaada wa mazishi.

Paschal alisema Malengo ya kavasha ni kuwahamasisha wanamuziki wajiunge na makundi rasmi kama mtandao wa wanamuziki, mifuko ya hifadhi ya jamii kama PSPF , NSSF pamoja na vikundi vya mtandaoni kama Kavasha group Tz ili kujiwekea akiba na pia kujirasimisha kwa ajili ya kurahisisha mambo mbalimbali ya kimaisha.

"Katoa wito kwa niaba ya kundi la Kavasha Group Tz kuwa linashauri familia ya muziki wa dansi nchini ni waimarishe Umoja na mshikamano ambavyo vitawafanya iwe rahisi kushirikiana na kuwa na nguvu moja katika masuala mbalimbali,"alisema Paschal.

Gama kwa sasa hana bendi amepumzika kutokana na maradhi ila aliwahi kupita bendi za Mchinga sound, Double M. Sound, Twanga Pepeta na nyinginezo.
Katika George Gama, pembeni kulia katibu wa Kavasha John Shekwavi na kushoto Mweka Hazina Tabu Mambosasa.