Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack  (kushoto) katika kijiji cha Wigelekelo wilayani Maswa ukitokea Kishapu Mkoani Shinyanga.
 Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akisoma taarifa ya Mkoa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2016, Ndg. George Mbijima katika kijiji cha Wigelekelo wilayani Maswa mara baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoani Shinyanga.

 Baadhi ya wasanii wa Ngoma ya Wagoyangi kutoka Maswa wakitoa burudani kwa kucheza ngoma wakiwa na nyoka aina ya chatu, mbele ya wananchi wa Wilaya hiyo waliofika katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika kijiji cha Wigelekelo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...