THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI NCHI AONGOZA WATUMISHI WA WIZARA YAKE KUAGA MWILI WA MWANASHERIA, MAREHEMU YUSTA MSOKA, JIJINI DAR

 Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akiaga mwili wa Mwanasheria wa Wizara hiyo, marehemu, Yusta Msoka, ambaye alifariki wiki iliyopita na mwili wake ulizikwa Mbagala, jijini Dar es Salaam jana. Nyuma ya Mapfa, ni Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Wizara hiyo, Jane Massawe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba, Afisa Sheria wa Wizara hiyo, Berious Nyasebwa wakiaga mwili wa mwanasheria mwenzao wa Wizara hiyo, marehemu, Yusta Msoka, ambaye alifariki wiki iliyopita na mwili wake ulizikwa Mbagala, jijini Dar es Salaam jana. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Lilian Mapfa (kushoto kwa Balozi), Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba wakiwa katika hali ya huzuni pamoja na waombolezaji wengine wakati wa kuaga mwili wa marehemu, Yusta Msoka, ambaye alifariki wiki iliyopita na mwili wake ulizikwa Mbagala, jijini Dar es Salaam jana.