THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

NAIBU WAZIRI MPINA AIADHIBU MANISPAA YA MJI WA TABORA

EVELYN MKOKOI -TABORA

Kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ameipa adhabu Halmashauri ya Maispaa ya Mji wa Tabora kwa kuitoza faini ya shilingi Milioni kumi na mbili na kutakiwa kulipa faini hiyo kwa muda wa wiki mbili, kwa kile kilichodaiwa ni kutokutii mamlaka za juu na kusema uwongo kuhusu hali ya usafi wa maingira ya mji wa Tabora.

Alipokoukuwa katika siku ya Pili ya ziara yake mkoani Tabora baada ya kupata taarifa ya hali ya mazingira ya mkoa huo, Na kuambiwa kuwa ni ya kuridhisha na kuwa DAMPO la mji huo ambalo siyo rasmi,lipo katika hali ya kuridhisha ndipo alipoamua kjutembelea DAMPO hilo na kujioea hali ya uchafu isiyovumilika kwa taka ngumu na hatarishi, kutomwagwa katika eneo husika na kuzagaaa barababarani.

Aidha kufuatia malalamiko ya wakazi wa mji huo, Mpina halikadhalika aliktembelea soko ya mji wa Tabora na kushuhudia Dampo katikati ya soko hilo lenye taka mbichi zenye harufu kali ambayo huweza kuhatarisha maisha ya watumiaji wa soko hilo kwa kupata magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Bw. Bosco Nduguru alisema ofisi yake ilikuwa na mpango wa kuhamishia soko hilo sehemu nyingine na kukubali changamoto zilijitokeza sokoni hapo na kuzifanyia kazi .

Wakati mwenyekiti wa soko hilo bwana Bakari Mpumila alieleza kuwa kuhamishwa kwa soko hilo hakuwezi kuwa suluhisho la kudumu kutatua changamoto za usafi wa mazingira kwani dampo linalotumika katikati ya soko hilo limekuwa ni kero iliyoshindikana toka kwa uongozi uliopita na Kumshukuru Naibu Waziri Mpina kwa ziara yake kwani ana imani kuwa sasa kero hiyo imeshatapatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Pamoja na kulipa faini hiyo manispaa pia inatakiwa kuondosha taka hizo a kumwaga kifisi cha molamu katika eneo hilo na kurekebisha mazingira ya choo sokoni hapo. 

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazngira Mhe. Luhaga  Mpina akiongea na maafisa na waaandishi wa habari alotangulizana nao katika DAMPO la mji wa Tabora na kushangazwa na hali halisi ya DAMPO hiyo na taarifa ya mazingira aliyopewa na mkoa kuhusu usafi wa mazingira wa mji wa Tabora.
Bw Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazngira Mhe. Luhaga Mpina akiongea na maafisa na waaandishi wa habari alotangulizana nao katika DAMPO la mji wa Tabora na kushangazwa na hali halisi ya DAMPO hiyo na taarifa ya mazingira aliyopewa na mkoa kuhusu usafi wa mazingira wa mji wa Tabora.