Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya leo amewasili Mkoani Kagera na kutembelea miundombinu ya sekta ya elimu ili kujionea namna serikali inavyorejesha hali kama awali kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea September 10 mwaka huu.

Akiwa katika shule ya sekondari ya Ihungo, Mhandisi Manyanya amewataka wakandarasi waliopewa dhamana ya kusimamia ujenzi upya wa majengo mapya ya Shule za Ihungo na Nyakato kujenga kwa kuzingatia viwango sahihi kulingana na maelekezo ya wataalam wa miamba.

“Mmepewa dhamana ya kusimamia ujenzi upya wa shule hii, nawaombeni muzingatie viwango sahihi wakati mnajenga hasa kwa kuangalia mapendekezo ya wataalam wa miamba waliyoyatoa ili kuyaweka majengo katika hali ya usalama” Alisema Mhandishi Manyanya.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu akimueleza Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya hatua zinazoendelea kuchukuliwa na serikali katika kurudisha hali baada ya tetemeko la ardhi kutokea mkoani huko.

Aidha Mhandisi Manyanya amewatahadharisha wakandarasi wenye tabia ya kudokoa vifaa vya ujenzi kutothubutu kufanya hivyo kwani yeyote atayeiba vifaa hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.
Katika kuhakikisha wanafunzi wenye ulemavu tofauti wanapata elimu sawa Mhandisi Manyanya amewataka walimu wa shule ya msingi Mgeza Mseto kutenda haki sawa wanafunzi wote bila kujali aina ya ulemavu alionao mwanafunzi.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akioneshwa baadhi ya majengo yatayojengwa upya katika shule ya sekondari ya Nyakato ambayo pia baadhi ya majengo yake yaliathiriwa na tetemeko la ardhi hiyo kuifanya kuamuliwa kujengwa upya.

Katika hatua nyingine Mhandisi Manyanya amezitaka shule hasa za sekondari nchini kuanzisha mashamba darasa yatakayowawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo shughuli za kilimo na kusaidia kuifanya shule kuwa na hifadhi ya kutosha ya chakula.

Kwa upande wa walimu Mhandisi Manyanya amewapongeza walimu wa wilaya ya Bukoba kwa kujituma na kuwekeza katika kilimo cha migomba na kuwataka walimu kote nchini kuiga mfano huo ili kuwa na chakula cha kutosha na kujiongezea kipato cha kuendesha maisha yao ya kila siku.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akimuonesha jambo mwanafunzi mwenye ulemavu katika shule ya msingi Mgeza Mseto iliyopo mkoani kagera alipoitembelea kuona namna ilivyoathiriwa na tetemeko la ardhi kwenye baadhi ya majengo yake.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...