Na Dotto Mwaibale

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philipo Mangula,amesema ameanza kupokea mafaili ya wana CCM ambao wameanza kujipitisha kutoa rushwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho unaotajariwa kufanyika mapema mwakani.

Mangula amesema ana  taarifa  kwamba wanaCCM wengi wameanza kutumia mbinu chafu za fedha kutaka nafasi mbalimbali na kwamba imekulakwao kwakuwa hawataweza kupenya atawashughulikia.

Mangula alitoa kauli hiyo alipokuwa akitoa mada ya maadili ya viongozi kwenye kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika katika Chu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam jana na kueleza kukerwa na tabiya ya wafanyabishara wenye fedha ya kutaka kuteka kila mahali.

Alisema ndani ya CCM nimaarufu kwa jina la mzee wamafaili, hivyo ataendelea kupitia mafaili hayo ilikuhakikisha maadili yanazingatiwa na kuenzi misingi yaAzimio la Arusha kwani hakuna atakayepenya kwa njia za rushwa.

“Zipo taarifa kuwa wapo baadhi wameanza kujipitisha na kutoa rushwa kwa ajili ya uchaguzi wa mwakani, nawahakikishia kwangu watu hao hawawezi kupitani tamfuatilia kila mmoja atakaye jihusisha na rushwa hapati nafasi hiyo,” alisema.

Alisema ili kudhibiti mianya hiyo atahakikisha sheria inatungwa ya kutenganisha kati  ya wafanyabiashara na uongozi kwa vile wafanyabishara wanatafuta nafasi ya uongozi ilikuendeleza biashara zao.

Mangula alisema ni aibu kwa mpiga kura kuhongwa kiasi kidogo cha pesa na kupoteza haki ya msingi ya kumchangua kiongozi mwenye sifa kwa ajili ya maendeleo.

 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (kulia), akihutubia wakati alipokuwa akifungua kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni  Dar es Salaam jana.
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (katikati), akisalimiana na wafanyakazi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere alipokuwa amewasili kwenye kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika chuoni hapo Dar es Salaam jana. Kushoto ni mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila. Manyanya alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo.
 Mgeni rasmi wa kongamano hilo Mhandisi Stella Manyanya (wa tatu kulia waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali walioshiriki kwenye kongamano hilo. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...