Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

NDEGE sita kufunika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius K. Nyerere katika ujio wa Mfalme wa Morocco Mohamed Vi akiongozana na wafanyabiashara 1000.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ziara hiyo ina manufaa kwa watanzania hivyo fursa ambazo zinaibuliwa kutokana ujio viongozi mbalimbali zitumiwe vizuri katika kujiletea manufaa.

Amesema kuwa ujio huo wa Mfalme wa Morocco utakwenda sambasamba na kusaini baadhi ya mikataba 11 kwa ikiwemo ya mahusiano, Reli ya Mchuchuma na Liganga, Uvuvi, Kilimo, utalii, siasa na mahusiano.

"Rais Dk. John Pombe Magufuli amekuwa akifanya kazi kwa ajili ya manufaa ya watanzania hivyo kila mtu atumie fursa hiyo kwa vitu vitakavyoibuliwa"Amesema Makonda.

Kutokana na ujio huo, watanzania wametakiwa kwenda kuulaki ujio wa kiongozi huyo ikiwa ni kuonyesha ukarimu wetu wenye amani.

Mkuu wa Mkoa huyo amesema Mfalme wa Morocco atazindua jiwe la msingi la ujenzi wa msikiti Bakwata.

Katika ziara hiyo wafanyabiashara watanzania watakutana na wafanyabiashara wa Morocco na kujifunza jinsi ya kushirikiana kibiashara kwa maendeleo ya taifa.

Ziara hiyo inatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 27 na kuondoka nchini saa 10 jioni
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya ujio wa Mfalme wa Morroco hapa nchini.Picha na Humphrey Shao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Translators mmewaandaa wa kutosha ili tuweze kuzitumia hizo fursa ? Wenzetu wanatumia zaidi kifaransa ns kiarabu sisi waswahili ni kibongo na kizungu Mh. MAKONDA upo hapo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...