Na Hussein Makame, NEC

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema itafikisha Elimu ya Mpiga Kura mpaka katika ngazi ya vijiji ili kuhakikisha wananachi wanaoishi vijijini wanapata elimu hiyo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani wakati akitoa Elimu ya Mpiga kura kupitia kipindi cha Hot Mix cha televisheni ya Afrika Mashariki (EATV) juzi usiku.

Bw. Kailima alikuwa akijibu swali la mtazamaji wa kipindi hicho aliyetambulika kwa jina moja la Jumanne, aliyeiomba Tume iwe na wafanyakazi wengi kwani Elimu ya Mpiga kura inahitaji kufika hadi vijijini.

Msikilizaji huyo alisema Elimu hiyo ni muhimu kwani hata mwananchi wa kijijini anaihitaji kwa kuwa anahusika katika kuchagua viongozi kwenye chaguzi mbalimbali nchini. Akijibu swali la mtazamaji huyo, Bw. Kailima alisema moja ya mikakati ya NEC kuwafikia wapiga kura kwa sasa, ni kuwatumia wenyeviti wa vijiji na tayari imeshaandika barua Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuiomba iiwezeshe Tume kutekeleza hilo.

Alisema Tume imeiomba TAMISEMI iipatie ratiba za mikutano ya kamati za halmashauri za mikoa, Wilaya na kamati za maendeleo za kata ambazo wajumbe wake ni wenyeviti wa mikutano mikuu ya vijiji ambao ni wenyeviti wa vijiji. “Kamati ya Halmashauri ya mkoa inakusanya watu wengi pale kwenye mkoa, tunataka tukawaelimishe pale.Katika mkutano mkuu wa kijiji mjumbe wake ni kila mwananchi mwenye umri wa miaka 18, kwa hiyo tutafika mpaka kwenye ngazi ile ya chini” alisisitiza Bw. Kailima na kuongoeza kuwa:

“Tuwaombe tu kwamba wakisikia Tume ipo kwenye mkutano wa kijiji kabla hawajaanza mkutamo wao, basi waje tuwasikilize.Lakini pia tutawafuata viongozi wa dini tuweze kutoa elimu ya mpiga kura”. Alibainisha kuwa kupatia viongozi wa dini, Tume itawaomba wanapojumuika kwa ajili ya ibada zao kwenye makanisa au misikiti waialike NEC iwaelimishe waumini wao kuhusu elimu ya mpiga kura.

“Kwa hiyo tutakwenda katika kila kona taratibu hadi kufikia mwaka 2020, Mungu akituweka hai nchi itabadilika na mwananchi atafahamu utaratibu mzima wa kuandikisha wapiga kura, kupiga kura na shughuli za Tume.” alisema Bw. Kailima. Alifafanua kuwa miakakati hiyo ikifanikiwa kutekelezwa itapunguza kwa kiwango kikubwa upotoshaji unaofanywa kuhusu mchakato wa Uchaguzi kwani wananchi watakuwa wanafahamu majukumu ya NEC na majukumu ya kwenye Uchaguzi.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatekeleza mikakati wa kutoa Elimu ya Mpiga nchi nzima na sasa inashiriki kwenye Wiki ya Vijana, Sherehe za Uzimaji wa Mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya Kifo cha Mwalimu. Julias Nyerere mkoani Simiyu. Hivyo Bw. Kailima aliwataka wananchi wafike kwenye banda la NEC kwenye uwanja wa Halmashauri ya Bariadi zinapofanyika shughuli hizo ili kuapata Elimu ya Mpiga kura inayotolewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...