Na. Aron Msigwa –NEC.Bariadi –Simiyu.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imepongezwa kwa kuanzisha programu endelevu  za utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura kwa kuwafikia wananchi moja kwa moja katika maeneo yao kote nchini.

Akitoa pongezi hizo mara baada ya kutembelea Banda la Maonesho la Elimu ya Mpiga Kura la NEC wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika Bariadi mkoani Simiyu,  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Muhagama amesema kuwa hatua ya NEC  kutoa elimu ya mpiga kura kupitia maonesho hayo inawasaidia wananchi kujifunza masuala mbalimbali kuhusiana na chaguzi za Tanzania.

“ Nawapongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuanzisha utaratibu huu wa kushiriki maonesho mbalimbali, mnafanya kazi nzuri, endeleeni hivyo hivyo kuwaelimisha wananchi” Amesema Mhe. Jenista.

 Ameeleza kuwa ushiriki wa NEC katika maadhimisho ya Wiki ya Vijana unawapa fursa vijana wengi kupata elimu sahihi kuhusu wajibu wao na majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kuratibu na kusimamia Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Kwa upande wake Afisa Habari wa Idara ya Elimu ya Mpiga Kura ya NEC Bi. Margareth Chambiri amwemweleza Waziri huyo kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanzisha program endelevu za kutoa elimu ya mpiga kura kwa kuhakikisha kuwa wananchi moja kwa moja katika maeneo mbalimbali nchini.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Muhagama (katikati) akikata utepe kufungua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Vijana leo mkoani Simiyu.   Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Anthony Mavunde, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka (wa pili kutoka kushoto), Waziri Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Titus Kamani na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Abdallah Possi (Mwenye Kofia).Picha na Aron Msigwa – NEC.
Wananchi wilayani Bariadi mkoani Simiyu wakipata elimu ya Mpiga Kura kwenye banda la Maonesho la NEC leo.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Muhagama akipata maelezo kuhusiana na Elimu ya Mpiga Kura alipotembelea Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo mkoani Simiyu.
 Baadhi ya Wanachi wakifuatilia ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere wilayani Bariadi mkoani Simiyu leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...