Na Humphrey Shao, Dar es Salaam

Baraza la mitahani nchini limeanzisha mfumo mpya wa Kutunza Kumbukumbu za Wanafunzi wa shule za Msingi (PREM), Utakaosadia uandikishwaji wa wanafunzi wote.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema jijini Dar es Salaam leo, Afisa Habari wa Baraza la Mitihani nchini, John Nchimbi, alisema kuwa mfumo huo utatoa namba Maalum ambayo itamtambulisha mwanafunzi katika ngazi zote za mitihani.

“Mfumo huu utakuwa na faida nyingi sana pamoja na kusaidia katika uhamisho wa mwanafunzi kutoka shule moja kwenda nyingine ndani ya mkoa au nje ya mkoa hivyo kuondoa tatizo la wanafunzi hewa”alisema Nchimbi.

Aliongeza kuwa mfumo huu utasaidia katika uandaaji na utoaji wa Takwimu za Wanafunzi katika ngazi ya shule Wilaya ,Mkoa mpaka Taifa.

Alimaliza kwa kusema kuwa Baraza limeanza kufanya majaribio ya Mfumo huu katika mikoa miwili ya Mwanza na Ruvuma na Ifikapo Disemba mfumo utaimarishwa ili Januari hadi Mei 2017 utumiwe nchi nzima kwa shule za msingi.
Afisa Habari wa Baraza la Mitihani nchini John Nchimbi akizungumza na wanahabari juu ya mfumo huo mpya. Kushoto ni Afisa Mitihani wa Baraza hilo, Khaflan Katiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...