THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

NEEC yawataka Wadau kutoa maoni kupata sera mpya

Katibu Mtendaji wa Baraza Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ((NEEC), Bi. Beng’i Issa, akifungua Jijini Dar es Salaam majadiliano ya tathimi ya Ripoti juu ya Sera ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mwaka 2004. (Kushoto) ni Afisa Mchambuzi wa Miradi (Program Analyst UN Women’s Economic Empowerment), Bi.Tertula Swai na (kulia) ni afisa kutoka baraza hilo, Bw. Edward Kessy.
Wadau kutoka taasisi za serikali na asasi za kiraia wakifuatilia taarifa ya tathimini ya Ripoti juu ya Sera Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya 2004 ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ((NEEC) katika mkutano wao Jijini Dar es Salaam jana. Tathimini hiyo iliwasilishwa na mwezeshaji wa Mkutano, Mchumi Mwandamizi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,Bw. Elias Luvanda (hayuko pichani).

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wanchi Kiuchumi (NEEC) limetangaza Jijini Dar es Salaam kwamba linaandaa sera mpya ya uwezeshaji wananchi kiuchumi  na limealika wadau kutoa maoni ili kupata sera itakayokidhi matakwa ya makundi yote katika jamii.

Akifungua mkutano wa majadiliaono tathimi ya Ripoti ya Sera ya Uwezeshaji Wananchi kiuchumi ya mwaka 2004 ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ((NEEC),Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Beng’i Issa, amesema baraza linawaalima wadau  kutoa mapendekezo yatakayosaidi kuandaa sera mpya badala ya sera ya sasa ya 2004.

SOMA ZAIDI HAPA