UMOJA wa Wafanyabiashara wa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Congo (DRC) Bw. Sumael Edward, ametangaza kurejea kwa wafanyabiashara wa nchi hiyo kutumia Bandari ya Dar es Salaam.
Bw. Edward alisema hayo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa iadara ya Habari Maelezo.
“Sisi kwa moyo mmoja tumeamua kurejea Bandari ya Dar es Salaam mara baada ya Baba zetu wote wawili Rais John Magufuli na Joseph Kabila kukubaliana mambo mazuri ambayo sisi kama wafanya biashara tunaona yana tija kwetu katika kukuza umoja wetu kati ya Tanzania na DRC”amesema Edward.
Aliongeza kuwa kwa sasa wanashukuru mizigo yao kwa sasa haikai bandarini kwa kuchelewa na hakuna ubabaishaji wa kupelekwa bandari pasipokuwa na lazima.
Alimaliza kwa kusema kuwa kwa sasa wananchi wa DR Congo wote wameanza kurejea Tanzania na biashara zote zitakuwa kama zamani na maduka yote Kariakoo yatapata wateja.
Rais wa Wafanyabiashara wa nchini DR Congo Bw. Sumael Edward akiongea na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam. Pembeni yake ni afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO, Bw. Tiganya Vicent.
Picha na Habari na Humphrey Shao wa Globu ya Jamii
Maneno mazuri humtowa nyoka pangoni. Pongezi za dhati kwa Marais wa pande hizo mbili kwa mazungumzo ya pamoja ikiwa ni katika kudumisha na kujenga uhusiano mzuri wa kimaendeleo khususan katika nyanja za kiuchumi na kibiashara mbali ya uhusiano wa karibu sana wa kiujirani na kindugu uliyopo kati ya Tanzania na DRC. Daima umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
ReplyDelete