Pichani ndege aina ya Boeing 747 iliyombeba Mfalme Mohammed VI wa Morocco na ujumbe wake ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jioni hii jijini Dar na kulakiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Pichani ndege aina ya Boeing 747 iliyombeba Mfalme Mohammed VI wa Morocco na ujumbe wake ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jioni hii jijini Dar na kulakiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake,Mfalme Mohammed VI kutoka Taifa la Morocco wakisimama pamoja wakati wa nyimbo za Taifa na mizinga 21 ikipigwa mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar jioni hii.Mfalme huyo amewasili jioni ya leo kwa ziara ya kikazi ya siku tatu,aidha imeelezwa kuwa Mfalme huyo aliyekuja na ujumbe wa watu takribani 1000,mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu,atakuwa na siku nyingine tano za mapumziko hapa nchini ambapo atatembelea maeneo mbalimbali ya vivutio na utalii nchini Tanzania.
Sehemu ya ujumbe wa wafanyabiashara waliotangulia kabla ya kutua kwa Mfalme Mohammed VI wa Morocco,aliyewasili jioni ya leo na kulakiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli na mamia ya wananchi.

Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ngoja tuone msimamo wa Tanzania kuhusu Sahara Magharibi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...