Mnamo Tarehe 26.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A mbeya day sec school aishie  Uyole alipigwa na walimu watatu,  Mwl Frank Msigwa, John Deo UDSM na Sanke Gwamaka wa Nyerere Memorial, wote wakiwa mafunzo.  

Mwl Frank alitoa assignment ya Kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwepo Sebastian hakufanya, darasani mwl alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo, ndio walimu wakamchukua na kumpeleka staff room na kuanza kumpiga vile. Tangu tar 29. September mwanafunzi hakuonekana shuleni. 

Na mwl Esther Harembo wa Iringa University ndio aliyekuwa akisema mwacheni mtamuumiza. Ndio aliyechukua video. Hao walimu wote hawapo wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao. 

POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali.Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo. 

MWIGULU Nchemba, W MNN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...