Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara, Bryceson Kibasa
akizungumza na wananchi wa Tafara ya Simbay kwenye uzinduzi wa mfuko wa afya ya
jamii iliyoboreshwa (iCHF) ambapo alisema wameboresha hospitali ya wilaya hiyo
Tumaini ikiwemo dawa kupatikana kwa wingi.
Meneja wa mfuko
wa Taifa wa Bima ya Taifa Nchini (NHIF) Mkoani Manyara, Henry Shekifu
akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Simbay Wilayani Hanang’ juu ya umuhimu wa
kujiunga na mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa (iCHF) ambapo huduma hizo
zitatolewa kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali zote za Serikali ndani
ya wilaya pia katika zahanati, vituo vya afya na hospitali binafsi na taasisi
za dini zilizo ndani ya wilaya na kusajiliwa.
Mkuu
wa Wilaya ya
Hanang’ Mkoani Manyara, Sarah Msafiri Ally akizungumza kwenye uzinduzi
wa mfuko
wa afya ya jamii ulioboreshwa (iCHF) wilayani hupo ulioratibiwa na ofisi
ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Manyara na kufanyika
katika Kata ya
Simbay ambapo wananchi wanapaswa kuchangia shilingi 30,000 na kutibiwa
kaya
moja yenye watu sita kwa mwaka mmoja.
Mkazi wa Tarafa
ya Simbay Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, Stephan Songay akizungumza kwa
kuwasisitizia wananchi wa eneo hilo kujiunga na mfuko wa afya iliyoboreshwa iCHF kwa
kuchangia shilingi 30,000 na kutibiwa bure kwa mwaka mmoja, kaya moja yenye
watu sita, baba, mama na watoto wanne ambao hawajatimiza umri wa miaka 18.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...