THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

NMB yazindua Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENKI ya NMB, imezindua Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani kwa kuahidi muendelezo wa huduma bora kwa wateja na kupokea ushauri kutoka kwa wateja na wadau, huku ikisisitiza utayari katika kuelekea Tanzania ya Viwanda.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika NMB Tawi la Msasani, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, amesema licha ya kuwa huduma bora ni kipaumbele cha kila siku, lakini wataitumia wiki hii kuboresha zaidi, ikiwamo kufanyia kazi maoni ya wateja.

Ineke amesema kwamba, kutokana na kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais John Magufuli, ya kuigeuza Tanzania kuwa ya viwanda, benki yake iko tayari kuendana na kasi ya mchakato huo, ambao unategemea sana ubora huduma za kibenki.

Ineke ameongeza , benki yake imekuwa kinara nchini sio tu katika utoaji wa huduma bora kwa wateja, bali pia huduma bora za kijamii kwa ujumla, ambako imekuwa ikichangia katika sekta zote, zikiwemo za afya na elimu.

Aidha, katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani, NMB imepanga kufanya ziara katika Kituo cha Kulelea Wazee kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambako pamoja na mambo mengine, watatoa msaada na kuhudumu kwa wazee waliopo kambi hiyo.

Ineke amewataka wateja wa NMB kuwa sehemu ya maendeleo ya benki hiyo kwa kutoa maoni yatakayoongeza kasi ya huduma bora, huku akiahidi kuyafanyia kazi maoni yote ya maboresho yatakayotolewa na wateja wao nchini kote.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker(Wapili kutoka kushoto) akizungumza na wateja waliofika asubuhi katika tawi la NMB Msasani na kuwaelezea malengo yao ya kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker akimkabidhi Godliver Mwendo cheti cha mfanyakazi bora wa benki hiyo katika uzinduzi a wiki ya huduma kwa mteja tawi la Msasani Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa tawi la NMB Msasani katika uzinduzi wa wiki ya huduma kwa mteja leo Jijini Dar es salaam.