Na Greyson Mwase, Lindi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa amewataka watumishi wanaofanya kazi katika kituo cha cha kupokea gesi kutoka Madimba na Songosongo kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam cha Somanga Fungu, kutunza mitambo na miundombinu ya mabomba ya kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ili kuepuka gharama za matengenezo ya mara kwa mara.

Profesa Ntalikwa alitoa rai hiyo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa kituo hicho katika ziara yake ya kukagua miundombinu ya gesi katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Alisema kuwa mitambo na miundombinu ya kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam kupitia Lindi na Pwani, inahitaji umakini wa hali ya juu katika uendeshaji wake pamoja na utunzaji ili mradi uwe na manufaa.

Alisema wananchi katika mikoa ya Lindi na Mtwara wanahitaji nishati ya umeme ya uhakika na kulitaka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuhakikisha linaweka mikakati ya kuhakikisha gesi inayozalishwa inatumika ipasavyo katika uzalishaji wa umeme.

“ Kutokana na kuwepo kwa nishati ya uhakika ya gesi, Tanesco mjipange kuitumia gesi hiyo kwenye mitambo yenu na kuhakikisha kuwa baadhi ya maeneo ya Lindi yanaondokana na adha ya kukatika kwa umeme,” alisema Profesa Ntalikwa.
Mtaalam kutoka kituo cha kupokea gesi kutoka Madimba na Songosongo kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam cha Somanga Fungu, Mhandisi Kelvin Kasian (kulia) akimwonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kushoto) mabomba ya gesi katika kituo hicho. (hayapo pichani).
Mabomba ya kupokea gesi kutoka Madimba na Songosongo kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam katika kituo cha Somaga Fungu kama yanavyoonekana pichani.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Mhandisi Kapuulya Msomba (kushoto) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (katikati) katika kituo cha kupokea gesi kutoka Madimba na Songosongo kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam cha Somanga Fungu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...