Muonekano wa kivuko kipya cha MV Kazi kikiwa katika hatua za awali za ujenzi wake. Kivuko hicho kinatarajiwa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akishuka kwenye pantoni mara baada ya kukagua utendaji wa kivuko cha MV. Kigamboni.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akisikiliza taarifa ya matumizi ya mafuta kutoka kwa Mhandisi wa Wakala wa Ufundi na Umeme  nchini (TEMESA) alipotembelea kivuko cha MV. Kigamboni.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameuagiza uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), kuhakikisha wanaweka mipango madhubuti ya kuongeza mapato katika vivuko vya MV. Kigamboni na MV. Magogoni kutoka Shilingi Milioni 14 ambazo zinakusanywa hivi sasa hadi kufikia Milioni 19 kwa siku.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kukagua vivuko hivyo na kuongea na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu Prof. Mbarawa amesema kuwa kipimo cha utendaji huo utafanyika ndani ya miezi minne ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa vivuko hivyo na kuweza kufikia malengo.

“Hatushindwi kutafuta mtu mwingine mwenye ujuzi na utendaji wa kazi uliotukuka, kama lengo la kukusanya milioni 19 halitafikiwa mkuu wa kivuko atafute kazi nyingine  na tutafanya hivyo mpaka tuhakikishe tunapata atayeweza kukusanya kiwango hiki”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...