Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisindikizwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016. Hii ni safari yake rasmi ya tatu kwenda nje ya nchi toka aingie madarakani mwaka mmoja uliopita. Alisafiri kwa mara ya kwanza alikwenda Rwanda, kisha akaenda Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Balozi wa Kenya nchini Mhe Boniface Muhia katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea saluti toka kwa Inspekta jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia wakati akipanda ndege kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na viongozi wengine wakipunga mikono kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati akianza safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016. PICHA NA IKULU
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...