Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika tamasha la madhehebu ya Bohora leo Oktoba 08, 2016,
ambayo yanafanya maadhimisho
ya dunia ya sikukuu ya mwaka mpya wa Kiislam Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 08 Oktoba, 2016
amehutubia katika tamasha la madhehebu ya Bohora ambayo yanafanya maadhimisho
ya dunia ya sikukuu ya mwaka mpya wa Kiislam Jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo
yamewaleta nchini wafuasi zaidi ya 30,000 kutoka nchi mbalimbali duniani na
kuongozwa na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna
Mufaddal Saifuddin Saheb (TUS).
Akihutubia wafuasi
wa Bohora katika Msikiti wa Hakimi uliopo Upanga Jijini Dar es Salaam, Rais
Magufuli amemshukuru Kiongozi Mkuu wa Bohora kwa kukubali kufanya maadhimisho
ya mwaka mpya wa madhehebu hayo hapa nchini na amewashukuru na kuwapongeza
wafuasi wa madhehebu hayo kwa kukubali kuja hapa nchini na kukaa kwa siku zote
za maadhimisho yaani kuanzia tarehe 02 Oktoba, 2016 walipoanza hadi tarehe 11
Oktoba, 2016 watakapomaliza.
Rais Magufuli, amewapongeza
viongozi na wafuasi wa madhehebu ya Bohora kwa kutumia maadhimisho haya
kuhimiza amani, upendo na mshikamano na pia amewashukuru kwa kushiriki katika
maendeleo ya kijamii na kiuchumi ikiwemo mchango Dola za Marekani 53,000
zilizotolewa na Kiongozi Mkuu wa Bohora kwa Serikali kwa ajili ya kuchangia
kampeni ya utengenezaji wa madawati, na kuwaleta madaktari kutoka Hospitali ya
Saifee ya India waliotoa matibabu bure kwa wananchi wa Arusha.
Aidha, Rais
Magufuli amewakaribisha wafuasi wa Bohora duniani kuja kuwekeza hapa nchini
katika sekta mbalimbali zikiwemo Kilimo, Uvuvi, Misitu, Mifugo, Madini na Gesi
kwani soko la uhakika lipo ndani ya nchi, katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) yenye watu takribani milioni 400.
Kwa upande wake
Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb (TUS)
amemshukuru Rais Magufuli kwa kuungana na wafuasi wa madhehebu ya Bohora katika
maadhimisho hayo na amesema wafuasi wote wa Bohora wanahimizwa kushirikiana na
mamlaka zilizopo katika nchi wanazoishi, kuwa raia wema na kufuata sheria.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es
Salaam
08 Oktoba,
2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akiwasili kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga
jijini Dar es salaam ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akisalimiana na Kiongozi wa Jumuiya ya
Mabohora Duniani, Dk Seydna Mufaddal Saifuddin mara alipowasili kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akihutubia mbele ya waumini na Kiongozi wa Jumuiya ya Mabohora Duniani, Dk Seydna Mufaddal Saifuddin kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam ambako
alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akiagana Kiongozi wa Jumuiya ya Mabohora Duniani, Dk Seydna Mufaddal Saifuddin kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016
Sehemu ya waumini kinababa kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016
Sehemu ya waumini kinamama na watoto kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016
mbona hakuna mipingo?
ReplyDeleteKwasababu shangazi yako hakualikwa pale na yeye ndiye mpambaji mkuu. Lakini pia wewe hukuwepo kama ungalikuwapo basi ungekumbuka kuiweka mipingo pale...
ReplyDeleteShangazi yangu hawezi itwa wala mimi siwezi itwa na rais kaitwa kwa sababu ni rais ili awasaidie matatizo yao lakini la sivyo blafrican hawezi kuwemo humo. sio mpaka waseme. data zimo pichani.
ReplyDeleteAngalia geographically mabohora wametokea wapi na mipingo inatokea wapi then tafuta link... Huu muingoliano wa mipingo na waarabu Ni link za kihistoria ikiwamo ukoloni ndio maana sisi hatuandiki wala kuongea kichina maana hatuna link...tuwaache mabohora wawatu
ReplyDeleteUkweli unabaki, hakuna mpangilio
ReplyDelete