THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

RAIS MAGUFULI AMKABIDHI VIFAA VYA UJENZI MJANE MKOANI KAGERA.


Na Eleuteri Mangi-MAELEZO.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemchangia vifaa vya ujenzi Mjane Agripina Angelo Mkazi wa Kitoma Wilayani Karagwe Mkoani Kagera.

Akimkabidi vifaa hivyo kwa niaba ya Rais, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu alisema kuwa Rais Dkt. Magufuli amefanya hivyo baada ya kuona kupitia vyombo vya habari jitihada za Mjane huyo kuanza kuijenga nyumba yake upya kutokana na kuharibika baada ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo mapema mwezi septemba.

Aidha Mkuu wa Mkoa Kijuu alitoa wito kwa wananchi ambao hawajaanza juhudi za kurejesha makazi yao waige mfano wa mjane huyo kwa kuanza ujenzi wa nyumba zao.Akizungumza baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo Bi. Agripina alisema kuwa anamshukuru Rais kwa mchango huo kwani vifaa hivyo vitamsaidia kukamilisha ujenzi wa nyumba yake na hatimaye kupata mahali pa kuishi yeye na familia yake baada ya nyumba yake ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi.

Vifaa alivyokabidhiwa mjane huyo ni pamoja na Mbao pisi 30, Mabati 35 ya futi kumi ,Saruji mifuko 25 ,Misumari ya mabati kilo 4, Misumari ya kenchi kg 7 na waya za kufungia makenchi kilo 3.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu akimkabidhi Vifaa vya ujenzi Mjane Agripina Angelo mkazi wa Kitoma Mkoani Kagera kwa Niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Mjane Agripina Angelo mkazi wa Kitoma Mkoani Kagera akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (Mst) Salum Kijuu nyumba aliyoijenga baada ya nyumba yake ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani kagera mapema mwezi September
Nyumba ya Mjane Mjane Agripina Angelo aliyoijenga baada ya nyumba yake ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani kagera mapema  mwezi September.SYLVESTER RAPHAEL-AFISA HABARI-KAGERA 


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. kutukamus Anasema:

    A great help to the one(s) in need indeed.