Jeshi la Polisi Tanzania, Kikosi cha Usalama Barabarani (T), Baraza la Usalama la Taifa Tanzania, kwa pamoja linatoa Shukrani nyingi kwako/kwenu kwa kujitokeza katika kusaidia Kikosi cha Usalama Barabarani, kutoa Elimu kwa Waendesha Pikipiki Maarufu kama Bodaboda, Kupitia Michezo Vijana mbalimbali zaidi ya 6,000 wameweza kupata Elimu kupitia Mashindano yanayoendela ya Mpinga Cup.

Hata hivyo ukiwa kama Mdau wa Michezo yetu ya Mpinga Cup 2016, tunapenda Kukufahamisha kwamba, Sasa tunaingia mzunguko wa pili baada ya kumaliza mzunguko wa kwanza.
Tulikuwa na Timu 128 zilizocheza hatua ya kwanza ya mtoano ambapo baada ya kucheza zimebaki timu 64 ambazo zinaanza mzunguko wa pili kwa njia ya mtoano.
mzunguko huu utafanyika kwenye Viwanja Vitatu vya KAMPALA GONGOLAMBOTO, VINGUNGUTI SHULE YA MSINGI NA BENJAMINI MKAPA SEKONDARI.
Inaanza tarehe 8/10/2016 na kumalizika tarehe 23/10/2016 na baada ya hapo tutabakiwa na timu 32 Bora zitakazocheza Raundi ya Tatu.Baada ya Raundi ya Tatu Tutabakiwa na Timu 16 Bora ambazo zitapewa Vifaa vya Michezo kwa ajili ya kucheza Ligi ya Mzunguko itakayokuwa katika Makundi mawili.

Tutapata Timu za Robo Fainali, Nusu Fainali na FAinali.
Kwa Kuwa Michezo ni Gharama kubwa na Pia Mahitaji ni Mengi, tunakuomba kwa Moyo wa Uzalendo uweze kujitokeza kwa mara nyingine kuweza kuchangia baadhi ya Mahitaji ili kuweza kufanikisha Mashindano yetu ambayo yameanza kwa ubora wa hali ya juu huku yakiwa pia ni mashindano ya kwanza kuandaliwa kwa kushirikisha timu nyingi kuliko 
mashindano yoyote Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...