THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

RC Arusha apokea mifuko 500 ya simenti na mabati 500 kutoka kwa kampuni ya ukandarasi ya Hanil JV Jiangsu kutoka Korea

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo amepokea mifuko 500 ya simenti na mabati 500 kutoka kwa kampuni ya ukandarasi ya Hanil JV Jiangsu kutoka Korea inayojenga barabara ya Tengeru - Sakina.

Msaada huo umetolewa ofisini kwake ambapo tukio hilo limeweza kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa,Wilaya na Wabunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Arusha.

Akipokea msaada huo, Mrisho Gambo amesema atagawa mifuko 100 ya simenti na mabati 100 kwaajili ya ujenzi wa Zahanati kata ya Murieti kwasababu kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wagonjwa katika hospitali ya Mkoa Mt.Meru wanaotoka maeneo hayo hivyo ujenzi huo utasaidia  kupunguza wagonjwa katika hospitali hiyo.

Pia yatakayo baki atayapeleka Wilaya ya Longido katika kusaidia ujenzi wa bweni la shule ya sekondari Longido ambayo liliungua moto nakuteketeza kila kitu.

“Napenda kuishukuru na kuipotengeza kampuni ya ukandarasi ya barabara ya Tengure Sakina na ile ya njia mbadala(by path) kwakutoa msaada huu na kwakuwa tumeshaanza  mkakati wa ujenzi wa madara kwa shule za msingi na Sekondari,hivyo nitagawa hayo mifuko ya simenti 100 na mabati 100 ikajenge Zahanati kata ya Murieti na yaliyobaki yataenda Longido katika ujenzi wa bweni lililoungua”.

Mkurugenzi  Mtendaji wa kampuni ya ukandarasi ya Hanil JV Jiangsu bwana Xie Jianbao amesema kampuni yao imetoa msaada huo ikiwa ni moja ya shughuli zao zakusaidia jamii katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

“Tumetoa mifuko ya simenti 500 na mabati 500 kama moja ya mchango wetu katika kusaidia jamii yetu kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo”.

Aidha Mkurungezi wa Jiji la Arusha,Athumani Kihamia alisema  kutokana na wingi wa wananchi waliopo katika kata ya Murieti Zahanati hiyo itaenda kuwasaidia sana na kwakipindi kisichozidi miezi 2 Zahanati hiyo itakamilika na wananchi wataweza kuitumia.

Ukosefu wa kituo cha afya katika kata ya Muriet ulibainika baada ya Mkuu wa Mkoa Gambo kufanya ziara katika kata hiyo nakupata malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa wanatembe umbali mrefu sana kutafuata huduma za afya.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akitoa shukrani kwa kampuni ya ukandarasi ya Hanil JV Jiangsu kwa kutoa msaada wa mifuko ya simenti 500 na mabati ya 500 kwa shughuli za maendeleo za Mkoa wa Arusha.
Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA