THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

RC Arusha Mrisho Mashaka Gambo, asiimamisha kazi watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo akitangaza kuwasimamisha kazi watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za uchaguzi wa mwaka 2015.
Watumishi hao ni pamoja na Bi. Hadija Mkumbwa ambae alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa mwaka 2015 na kumfuta cheo hicho,bwana Evansi Mwalukasa alikuwa mwekahazina wa halmashauri na  bwana Sembeli Sinayo yeye alikuwa mwanasheria wa halmashauri.
Maamuzi hayo yamefikia baada yakubainika kuna upotevu  wa fedha za uchaguzi takribani Milioni 188 ambazo matumizi yake hayakuwekwa  wazi na pia Milioni 20 zilitumika kwa manunuzi ambayo hayakufuata taratibu za manunuzi ya serikali.
“Kuanzi sasa nawasimamisha  kazi hawa watumishi watatu kwasababu wameisababishia serikali hasara ya takribani Milioni 128 ambazo zilikuwa fedha za uchaguzi”.
Aidha Mhe. Gambo alisema maamuzi hayo yametokana na taarifa aliyokabidhiwa na kamati aliyoiunda ya kuchunguza mapato na matumizi ya fedha za halmashauri hiyo na kubaini upotevu huo wa fedha nyingi ambazo amesema zingeweza kusaidia shughuli mbalimbali za uchaguzi katika Wilaya hiyo.
Amsema  fedha nyingine zimetumika kwenye manunuzi ambayo hayakufuata taratibu na sheria za manunuzi ya serikali  kinyume kabisa na taratibu za serikali katika maswala ya manunuzi.
Mhe. Gambo pia kasisitiza  watumishi wa serikali kufuata taratibu, sheria na kanuni mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao ili kuepuka migongano na uvunjifu wa sheria mahala pa kazi na kupelekea kupoteza ajira  zao.
Watumishi wa Halmashauri ya Ngorongoro, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (hayupo pichani) alipokuwa akitoa taarifa ya kamati ya uchunguzi aliyoiunda kuchunguza mapato na matumizi katika halmashauri hiyo.