THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

RC Gambo aongoza Kikao cha 38 cha bodi ya barabara cha Mkoa wa Arusha leo

Rais Dkt John Pombe Magufuli ameandika historia kwa wananchi tangu Tanzania ipate uhuru na kuelekea kutimize mwaka 1 madarakani kwa kuipatia Wilaya ya Ngorongoro  barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 60 tangu Wilaya hiyo ianzishwe.

Haya yameelezwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakati wa Kikao cha 38 cha bodi ya barabara cha Mkoa huo.
Gambo alisema  barabara hiyo inayotarajiwa kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami  na itaunganisha  mji wa Wasso hadi Sale kilomita 60 imepata Baraka zote kutoka kwa Rais Magufuli.

Gambo ameeleza katika Kikao  hicho kwamba  Rais Magufuli ameagiza kuanza kujengwa kwa barabara hiyo mara moja  kwa kiwango cha lami kama alivyoahidi wakati wa Kampeni alipokuwa katika Wilaya hiyo.

Amesema barabara hiyo  inatarajiwa kutekelezwa na Wakala wa barabara mkoani Arusha ( TANROADS).

Mkuu huyo wa Mkoa amesema  hii ni hatua muhimu sana kwa Wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro ,Wilaya  haina hata barabara moja yenye kiwango cha lami.

Mkuu huyo wa Mkoa pia alisema  fedha zinazotolewa na wafadhili benki ya dunia  sio msaada  bali ni fedha za mkopo kwa Tanzania ambazo  Tanzania italazimika kuzilipa hapo baadaye.

Akitoa shukrani zake mbunge wa jimbo la Ngorongoro Tate William Ole Nasha alisema kwa mala ya kwanza Ngorongoro inapata barabara yenye kiwango cha lami, kweli itakuwa furaha kubwa sana kwa wananchi wa Wilaya hito.

Wilaya ya Ngorongoro ni kati ya Wilaya sita za Mkoa wa Arusha  ambapo Wilaya hii inakabiliwa na matatizo makubwa ya miundo mbinu ya ukosefu wa barabara za uhakika ambapo usafiri katika Wilaya hiyo ni wa kubahatisha kutokana na kukosekana kwa miundo mbinu ya uhakika ya barabara kwenda maeneo ya vijijini.

Hivi sasa TANROADS inahudumia kiasi cha kilomita 1,220 katika Wilaya   za Mkoa wa Arusha zikiwemo  barabara kuu na barabara za Mkoa alisema Meneja wa Mkoa Mhandisi  John Kalupale.
Wajumbe wa bodi ya barabara ya Mkoa wa Arusha waliohudhulia kikao cha 38 cha bodi hio,jijini Arusha.