THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

RC GAMBO AWAACHIA TABASAMU WANANCHI WA TERRATI – ARUSHA


Nteghenjwa Hosseah – Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amechangia Lita 600 za mafuta kwa ajili ya greda la Halmashauri ili liweze kutengeneza miundombinu ya barabara kwenye maeneo yote korofi yanayozunguka kata ya Terrati.

Rc Gambo amefanya hivyo wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Terrat uliofanyika kwenye Shule ya Msingi Terrat wenye lengo la kufahamu changamoto za muda muda mrefu zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.

Katika Mkutano huo Mkuu wa Mkoa alianadamana na watalaamu wa Taasisi mbalimbali zinazotoa huduma katika Mkoa huu pamoja na menegiment ya Jiji ili kuwezesha upatikanaji wa majawabu ya kero zote zilizo wasilishwa na wananchi hao ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa haraka ili kumaliza kabisa changamoto hizo.

Wananchi wa Kata hiyo wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na kero ya ubovu wa miundombinu ya barabara, kukosekana kwa maji safi na salama pamoja na umeme katika eneo hilo na pia walitoa shukrani zao kwa Mkuu wa Mkoa kwa kuwapa kipaumbele katika ziara zake za kutambua changamoto za Mkoa wake.

Sisi wakazi wa huku tumekua kama hatuishi kwenye Jiji la Arusha kwa sababu huduma zote muhimu zimekuwa kikwazo sana kwetu mpaka zinasababisha kudorora kwa uchumi kwa wakazi wa maeneo haya kwa kuwa hapavutii wafanyabiashara kuja kuwekeza wala wanunuzi kutoka mjini hivyo tumekua tukiuziana sisi kwa sisi ambao wote tuna vipato duni alisema Jumanne Juma Kingu.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa Jina la Eliakim Mason kutoka Mtaa wa bondeni kati alisema kuwa Gari lakubebea wagonjwa katika kituo cha Afya Mkonoo limeharibika kwa kipindi kirefu sana na wanapata tabu ya kusafirisha mgonjwa hadi kufikia kwenye Hospital za Mjini Arusha inawalazimu kukodi Gari kwa gharama kubwa ili kunusuru maisha ya ndugu zao pia alilalamikia uhaba wa watumishi katika Kituo cha Afya Mkonoo na kudai kwamba inakuwa vigumu kupata hudma bora wagonjwa wanapokua wengi katika kituo hicho. 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kwanza kulia) akizungumza na wananchi wa Kata ya Terrati kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Mkonoo. 
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Terrati waliohudhuria Mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha 
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Kihamia (aliyesimama) akiwatambulisha wakuu wa Idara za Jiji (hawapo Pichani) kwenye Mkutano wa hadahara. 
Mhandisi wa barabara Jiji la Arusha Fordia Mwankenja (anayepunga mkono) akiwasalimia wananchi wa Kata ya Terrari kwenye Mkutano wa hadhara 
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Gabriel Daqarro akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuzungumza na wananchi wa Kata ya Terrati kwenye Mkutano wa hadhara.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilaitayoki Mhe. Long’ida Lomayani Kupitia Chadema akiwasilisha kero za mtaa wake kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha