Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika mkutano wa
hadhara uliofanyika leo jioni katika eneo la Buguruni kwa Mnyamani, ili
kuzungumzia kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Katika
Mkutano huo Makonda amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele katika
kuhakikisha wanashiriki katika kupunguza au kuondoa kabisa changamoto
zinazowakabili ikiwemo, vibaka, dadapoa na uchafu wa mazingira, akisema,
ikiwa wananchi watashitiki kikamilifu ni rahisi kukomesha tatizo la
vibaka kwa sababu vibaka na dadapoa wanatoka miongoni mwa familia zao na
hali kadhalika uchafu wa mazingira unatokana na takataka wanazozalisha
wananchi wenyewe.
Kamanda wa Polisi Kanda Malum ya Dar es Salaam, Simon Sillo akijibu hoja, kero na changamoto mbalimbali walizouliza wananchi, katika mkutano wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, uliofayika leo jioni Buguruni kwa Mnyamani
Viongozi
waandamizi katika Wilaya ya Ilala, wakimsikiliza mkuu wa mkoa Paul
Makonda wakati akihutubia wananchi katika eneo la Buguruni kwa Mnayamani
leo jioni. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela
Palela, Ofisa Tawala wa Manispaa hiyo, Edward Mpogolo, Naibu Meya
Manispaa hiyo, Omary Kumbilamoto na Mbunge wa Segerea wilayani humo Bona
Kalua
Mjumbe
wa Shina namba tano, Katika Kata ya Myamani, Buguruni Zubeda Lugiga,
akieleza kero zinazowakabili wakazi wa kata hiyo, mbele ya Mkuu wa mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipowahutubia katika mkutano wa hadhara
leo jioni
Mkazi
wa Buguruni, Sadik Mgaya akieleza changamoto na kero zinazowakabili
wananchi wa eneo hilo wakati wa mkutano huo wa Makonda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...