Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wazazi na walezi kuwaacha huru watoto wao kuendelea na masomo wayapendayo badala ya kuwachagulia.

Mwito huo ameutoa katika mahafali ya 32 ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Jitegemee JKT Mgulani Dar es Salaam jana ambapo alikuwa mgeni rasmi.

"Watoto wapewe uhuru wa kile wanachopenda kukisomea badala ya kuwachagulia kwa kufanya hivyo itawasaidia kupenda kazi watakayoifanya kutokana na masomo waliyosoma" alisema Makonda.

Alisema hivi sasa kuna changamoto kubwa kwa watumishi kujiingiza katika vitendo vya ubadhirifu kutokana na kutokuwa wazalendo kutokana na kufanya kazi ambayo imetokana na masomo ambayo hawakuyapenda.

Alisema kama mtoto anapenda kuwa mtaalamu wa kompyuta muache aendelee na masomo ya kompyuta badala ya kumlazimisha kuwa na taaluma nyingine.

Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy alisema wahitimu hao wameandaliwa vizuri kwa ajili ya kufanya mtihani wao watakao uanza Jumanne wiki ijayo na kuwa wanategemea wote watafanya vizuri.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT Mgulani katika mahafali ya 32 yaliyofanyika jana. Makonda alikuwa mgeni rasmi. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo, Brigedia Generali Laurance Magere.
RC Makonda akimkabidhi cheti Mwalimu Bora wa Shule hiyo, Grace Eliyatosha Moshi.
RC Makonda akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Bora,  Samuel Ndebeto.
Mkuu wa Mkoa Paul Makonda (katikati), akiwa meza kuu na viongozi mbalimbali. Kutoka kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Kigamboni, Luteni Kanali, Laurent Mgongolwa, Mkurugenzi wa Mipango ya Huduma Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Festus Mang'wela, Mkuu wa Shule ya Sekondari Jitegemee, Luteni Kanali, Robert Kessy, Mwenyekiti wa Bodi wa shule hiyo, Brigedia Generali mstaafu, Laurence Magere, Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Hashim Komba na Mjumbe wa Bodi wa Shule hiyo, Sebastian Enosh.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...