THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Samsung yazindua kiyoyozi chake kipya

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Samsung Afrika Mshariki, Nandakishore Nair (kulia) akipiga makofi mara baada ya Rais wa Chama cha Wabunifu Majengo, Henry Mwoleka kukata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa bidhaa hizo uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro Dar es Salaam jana.
Rais wa Chama cha Wabunifu Majengo, Henry Mwoleka na (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Samsung Afrika Mshariki, Nandakishore Nair wa pili (kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa Afisa masoko wa Kampuni ya Samsung, Mhandisi, Meshack Odhiambo mara baada ya uzinduzi wa AC mpya za Kampuni ya Samsung iliyofanyika katika Hotel ya Hayatt Kilimanjaro Dar es Salaam jana. 

Kampuni ya Kielektronikia ya Samsung Afrika Mashariki, imezindua kiyoyozi chake kipya chenye vifaa vya 360 Cassette, DVM Chiller, next generation DVM S 30 HP, pamoja na kifaa cha pembeni cha kutolea maji/hewa (VRF unit) – the DVM S Eco 14 HP.

Kwa pamoja, huu ubunifu wa hivi vifaa vipya (360 Cassette, DVM Chiller, next generation DVM S 30 HP, pamoja na kifaa cha pembeni cha kutolea maji/hewa (VRF unit) – the DVM S Eco 14 HP) utabadili hali ya sasa ya viyoyozi hususani kwenye ongezeko la nishati, ufanisi na utendaji, uchukuaji mdogo wa nafasi pamoja na kuongeza kasi ya upatikanaji wa ubaridi.