Na Benedict Liwenga-MAELEZO.

Serikali imepanga kuijenga shule ya msingi ileega na kufanya ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Nyamilima zote zilizopo wilayani kyerwa mkoani Kagera kufuatia uharibifu uliotokana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani huko mapema mwezi September.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya alipofanya ziara wilayani huko kuangalia athari za tetemeko katika sekta na elimu.

Mhe. Manyanya alisema kuwa kama serikali imejikita katika kurudisha miundombinu ya umma ikiwemo shule ili kuwawezesha wanafunzi kuendelea na masomo kama kawaida.

“Tumeona hali ni mbaya kwenye shule hizi mbili na sisi kama serikali hatuwezi kuliacha suala hili lazima tuzikarabati na kuzijenga zile zinazohitaji kujengwa upya na dhumuni ni kuhakikisha wanafunzi wanaendelea na masomo na kuondokana na changamoto hii: Alisema Mhandisi Manyanya.

Aidha Mhandisi Manyanya amemtaka mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Nyamilima kuacha tabia ya kutoa ruhusa hovyo kwa walimu suala ambalo linaathiri taaluma kwa wanafunzi.

Wakati huohuo Mhandisi Manyanya amesema walimu watakaoshindwa kuwawezesha wanafunzi wao kujua kusoma na kuandika watashushwa vyeo.

Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya (wa pili kushoto) akitoa maagizo kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Nyamilima Bw. Josam John (mwenye shati la maua) baada ya kugundua kuwa baadhi ya Walimu wa shule hiyo wamekuwa na tabia ya kuomba ruhusa mara kwa mara wakati wa saa za kazi.
Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya(kulia) akimpa fedha kama zawadi mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyamilima iliyopo Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera kwa kuweza kusoma na kuandika vizuri wakati alipowatembelea kuwapa pole kwa kukumbwa na tetemeko la ardhi

Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng. Stella Manyanya pamoja na Viongozi wa Serikali na Walimu wa Shule ya Msingi Ileega wakiangalia nyumba ya Walimu iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi kipindi cha hivi karibuni Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...