Serikali imeyakabidhi makampuni ya mafuta ya OILCOM, GBP na MOIL hati za Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Nyakato iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardhi mkoani Kagera lilitokea mwezi Septemba mwaka huu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano wa hati hizo jijini Dar es Salaam leo Tarehe 23 Oktoba, 2016, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Dkt. Hamisi Mwinyimvua ameyashukuru makampuni hayo kwa ahadi ya kujenga shule mbili zilizobomoka kutokana na tetemeko hilo.
“Shule ya sekondari ya Ihungo na Shule ya Sekondari ya Nyakato zilibomoka kutokana na tetemeko hilo, Kwa kuwa serikali imeanza kujenga shule ya sekondari ya Ihungo ninawakabidhi nyaraka za ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyakato na ninaamini mtakamilisha ujenzi kwa wakati ili wanafunzi waweze kurejea shuleni hapo”amesema Mwinyimvua
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, Sharif Mansoor amesema makampuni yao yataendelea kuziunga mkono juhudi za serikali za kukabili na kurejesha hali pindi maafa yanapotokea nchini.
“Sisi tunaamini nchi yetu ya Tanzania lazima ijengwe na watanzania wenyewe na sisi hatunabudi kuwasaidia ndugu zetu wa Kagera kwa athari walizozipata za tetemeko kwa kujenga shule hiyo kwa ramani ambayo mmetukabidhi” amesema Mansoor
Naye, Katibu Mkuu wizara ya elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Bi. Maimuna Tarish amesema kuwa jukumu la wizara hiyo ni kutoa elimu bora na ili elimu iwe bora ni lazima iwepo miundo mbinu ya majengo ya shule ambayo ni bora kama itakayojengwa na makampuni hayo ya mafuta.
“Tutawakabidhi michoro ya shule hiyo ambayo ujenzi wake umezingatia ushauri wa wataalamu wakiwemo wa Jiolojia, aidha katika ujenzi  mtakao kuwa mnaufanya Wakala wa majengo ya serikali (TBA), itasimsmia kazi ya ujenzi ili kuhakikisha ubora unaotakuiwa unafikiwa” amesema Tarish
Itakumbukwa kuwa nchi yetu ilikumbwa na tetemeko la ardhi katika Kanda ya Ziwa na Hasa Mkoa wa Kagera , Mwezi Septemba mwaka huu. Tetemeko hilo lilikuwa na athari kubwa kwa miundombinu na majengo ya taasisi mbalimbali za serikali na makazi ya wananchi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMAPILI, OKTOBA 23, 2016

h1
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge), Dkt. Hamisi Mwinyimvua akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, Sharif Mansoor , hati za ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyakato,  kutokana na hiyo na  makumpuni ya mafuta mengine ya OILCOM na GBP waliahidi kuijenga shule hiyo iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardh mkoani Kagera, Septemba, 2016, makabidhiano hayo yamefanyika tarehe, 23 Oktoba jijini Dar es salaam.
h2
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge), Dkt. Hamisi Mwinyimvua akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, Sharif Mansoor , hati za ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyakato iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardhi mkoani Kagera Septemba , 2016, kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu GBP Badal Sood, Mkurugenzi MOIL, Altaf Mansoor, kushoto kwake ni Katibu Mkuu wizara ya elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi,Maimuna Tarish, tarehe, 23 Oktoba jijini Dar es salaam. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...