Serikali imesitisha kwa muda zoezi la upigaji chapa kwa ng’ombe ili kutoa fursa kwa wadau kujadiliana na kuona namna bora ya la utekelezaji wa zoezi husika na kukabiliana na changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi iliyosainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bernard Kaali inasema kuwa zoezi hilo limekuwa likitekelezwa katika baadhi ya mikoa kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Taarifa hiyo inasema kuwa zoezi hilo limetokana na sheria Na 10 ya mwaka 2010 ya utambuzi, uandikishaji na utafitiliaji wa mifugo nchini, ambapo sheria hiyo inalenga kuhakikisha ufugaji unakuwa na tija kwa kuwezesha mifugo na biidhaa zake kupenya kwenye masoko ya kimataifa.

Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa sheria hiyo inasaidia katika kutatua changamoto ya migogoro baina ya wafugaji na watuamiaji wa ardhi pamoja na kudhibiti masuala ya wizi na kuenea kwa magonjwa ya mifugo.

Pia inasema kuwa Sheria hiyo inatekeleza uhitaji wa masoko ya kimataifa ya kuwezesha kufuatilia bidhaatoka kwa mlaji hadi kwa mzalishaji hivyo endapo zoezi hilo litatekelezwa na wadau na viongozi wa ngazi zote litakuwa na manufaa kwa wafugaji na taifa kwa ujumla na kupelekea kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo.

Hata hivyo zoezi hilo limesitishwa kwa muda muda ili kutoa nafasi kwa Wizara na wadau ikiwemo Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na wafugaji kujipanga ili kutekeleza ubora na ufanisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...