·          *Vitatumika kwa wanaonza masomo na wanaoendelea

Serikali imetangaza vigezo vitakavyotumika katika kupanga na kugawa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka 2016/2017 vitakavyotumika kwa wanafunzi wa mwaka wa kwaza na wale wanaoendelea.

Akizungumza na waandishi wa habari jioni ya leo (Ijumaa, Oktoba 14, 2016) katika Ofisi za Bodi ya Mikopo (HESLB) zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya amesema vigezo hivyo vinazingatia mahitaji ya kitaifa, uhitaji wa waombaji na ufaulu katika kozi za kipaumbele.

“Kozi za kipaumbele ni kama fani za sayansi za tiba na afya, ualimu wa sayansi na hisabati, uhandisi wa kilimo, gesi na mafuta na nyinginezo,” amesema Naibu Waziri Manyanya.

Kwa mujibu wa Mhandisi Manyanya, fani hizi zinatokana na mahitaji ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 ambazo zinasisitiza umuhimu wa kuzalisha watalaamu wanaokidhi mahitaji ya kitaifa katika fani hizo.

Naibu Waziri huyo ametaja vigezo vingine kuwa ni uhitaji wa waombaji hususani wale wenye mahitaji maalum kama wenye ulemavu na yatima.

Aidha, waombaji wenye ufaulu wa juu na wanachukua kozi za kipaumbele nao watafikiriwa, amesema Naibu Waziri Manyanya katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Maimuna Tarishi na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru.  

Kuhusu kutolewa kwa orodha ya waombaji waliofanikiwa kupata mikopo kwa 2016/2017, Naibu Waziri huyo amesema Bodi imekamilisha uchambuzi wa majina ya waombaji ambao wana sifa zilizoainishwa hapo juu na majina ya wanufaika wapya yatatangazwa leo tarehe 14 Oktoba, 2016.

Aidha, kuanzia mwaka huu wa masomo, wanufaika wote wa mikopo (wapya na wanaoendelea na masomo) watakopeshwa kulingana na uwezo wao (means tested) katika vipengele vyote vya mikopo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...