THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

SERIKALI YATOA MIEZI 3 KUONDOA MAKAZI YALIYOJENGWA KARIBU NA SHULE,VITUO VYA AFYA,MAENEO YA MASOKO

Na Bakari Issa Madjeshi,
Globu ya Jamii

Serikali imeagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya Kusimamia zoezi la kuondoa makazi ya Watu waliojenga karibu na Shule za Msingi, Sekondari, Zahanati, Vituo vya Afya na Maeneo ya Masoko kwa kile kilichoelezwa kuwa ni usumbufu na kuondoa utulivu katika maeneo hayo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mhe. George Simbachawene (pichan) amesema katika maeneo hayo kuna uvamizi tofauti ikiwa ujenzi wa Nyumba za Kufanyia biashara.
Mhe Simbachawene amesema upo uvamizi mwingine ambao ni uporaji wa ardhi iliyotengwa kwa ajili ya Shule, Zahanati mijini na vijijini.
Mhe. Simbachawene ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na serikali kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa juu ya Uvamizi huo kwa kuonyesha alama za mipaka ya maeneo hayo.
‘’Wakurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa waanzishe zoezi la kubainisha mipaka ya asili ya maeneo yote na kuyapima kuhakikisha yana Hati Miliki’’, amesema Mhe. Simbachawene