THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

SERIKALI YATOA TAMKO KWA WATUMISHI WA UMMA KUJITOKEZA KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA KABLA YA OKTOBA 31, 2016

Serikali imewataka watumishi wote nchini walioajiriwa na Serikali, yakiwemo mashirika ya Dini na Taasisi  nyingine ambazo haziko kwenye orodha ya malipo ya mishahara ya Serikali lakini zinapata ruzuku kutoka Serikalini; kuwa wamesajiliwa katika zoezi  la Vitambulisho vya Taifa kwa Watumishi wa Umma linaloendelea kote nchini, kufikia Oktoba 31, 2016.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angellah J. Kairuki (Mb) alipozungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, katika mkutano wa pamoja ulioitishwa kati ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Waziri ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Bi Kairuki amesisitiza; “waajiri na watumishi watakaoshindwa kutekeleza zoezi hili watachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo”
Akifungua mkutano huo uliolenga kutoa tathmini ya mwenendo  wa zoezi linaloendelea la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa Watumishi wa Umma lilioanza nchi nzima tangu Oktoba 03, 2016, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu L. Nchemba (Mb) amesema mpaka sasa Mamlaka ya  Vitambulisho vya Taifa (NIDA)  imefanikiwa kusajili zaidi ya asilimia 50% ya watumishi wote nchi nzima na baadhi ya mikoa kukamilisha usajili kwa zaidi ya asilimia 95%. Ameutaja mkoa wa Geita kuwa mkoa unaoongoza kwa kufanya vizuri katika zoezi hilo
Amesema pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali zilizokwamisha zoezi hilo kukamilika kwa wakati uliopangwa; Wizara yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, wameamua kuongeza muda wa kukamilisha zoezi hilo kwa wiki mbili zaidi hadi Oktoba 31, 2016.
Amewataka watumishi kuondokana na upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watumishi kwamba zoezi hilo limelenga kuhakiki vyeti na badala yake wajitokeze kwa wingi kusajiliwa kwani Serikali imelenga kuunganisha taarifa za mfumo wa mishahawa wa Serikali na NIDA, ili mbali na kutatua tatizo la watumishi hewa; kupitia mfumo huu wa kielektroniki unaomtambua mtu kwa alama zake za kibaiolojia kuwa na maslahi mapana kwa taifa na kwa watumishi; kwa kuunganisha mifumo mingine ya Serikali ukiwemo mfumo wa Kodi, mifuko ya Hifadhi za Jamii, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Bima ya Afya, Uhamiaji, RITA Na Benki ili kutoa manufaa mapana kwa mtumishi.
Amelipongeza Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kuwezesha kusambazwa kwa vifaa vya usajili nchi nzima, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Taasisi na Mashirika yote ya Serikali waliojitoa kufanikisha zoezi la Usajili.
Kupitia zoezi la Usajili Watumishi wa Umma, Tayari NIDA imefungua ofisi za usajili nchi nzima, ngazi ya Wilaya kusogeza karibu zaidi huduma inayotolewa kwa wananchi. Kwa mujibu wa Waziri Mwigulu Pindi zoezi  la usajili watumishi litakapokamilika usajili wa wananchi utaanza mara moja nchi nzima kwani zoezi la usajili vitambulisho vya Taifa limelenga kila mwananchi, Mgeni anayeishi kihalali nchini na Mkimbizi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu L. Nchemba (Mb) akizungumza wakati wa mkutano na vyombo vya habari mkoani Dodoma kuhusu mwenendo wa zoezi linaloendelea la usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa Watumishi wa Umma. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angellah J. Kairuki (Mb) na Bi. Rose Mdami, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati, akimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu L. Nchemba (Mb) Akisisitiza jambo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu zoezi la kusajili watumishi wa Uma nchi nzima. kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angellah J. Kairuki (Mb) na kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu L. Nchemba akipokea maelezo ya namna shughuli za usajili zinavyo ratibiwa na ofisi ya usajili Wilaya ya Dodoma Mjini ; alipofanya ziara ya ukaguzi na kukutana na viongozi na watumishi wa Umma waliofika kupata huduma