Na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza,

Jeshi la Magereza nchini kupitia Shirika lake la uzalishaji mali (Prisons Corporation Sole) limeingia Makubaliano na Mfuko wa Jamii wa PPF katika ujenzi na uboreshaji wa mradi wa Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga – Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Makubaliano hayo yamefanyika leo Jumanne 04 Oktoba, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano ulioko Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na Wanahabari, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Minja amesema uhirikiano huo unalenga kuliimarisha Shirika la Magereza ili liweze kujiendesha kibiashara pamoja na kuchangamkia fursa mbalimbali za kibiashara.

Kamishna Jenerali Minja ameongeza kuwa uwekezaji katika kiwanda hicho utalisaidia Jeshi la Magereza kufikia kiu ya kuzalisha bidhaa za ngozi zenye ubora wa hali ya juu na zinazochochea ushindani katika soko la ndani na nje.

“Naamini uwekezaji huu wa Kiwanda kipya cha Viatu cha Karanga Moshi ni ishara tosha ya kuunga mkono dhamira ya dhati ya Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli ya kutaka Tanzania mpya ya Viwanda inawezekana hivyo kutimiza malengo na Dira ya Taifa ya Uchumi wa Viwanda ifikapo mwaka 2025”. Alisema Kamanda Minja.

. Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio wakibadilishana nyaraka mbalimbali za Makubaliano katika Mkataba huo kama inavyoonekana katika picha. 
Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio na Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) wakionesha nyaraka mbalimbali baada ya hafla fupi ya utiwaji saini wa Mkataba wa ujenzi wa Kiwanda kipya cha Viatu. 
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakishuhudia utiwaji wa Mkataba huo kama inavyoonekana katika picha(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza). 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...