Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) unatarajia kukabidhi mchango wa maafa ya tetemeko la ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Kagera baada ya siku ya awali iliyokuwa imepangwa ya Oktoba 14, 2016 ya maadhimisho ya kumbukumbu ya kfo cha Mwalimu Nyerere kuingiliana na ratiba nyingine za kitaifa. 

Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib akizungumza katika mkutano wa wanachama jana alisema mpaka sasa fedha ambazo zinatarajiwa kukabidhiwa ni sh. 600,000 ambazo kati ya hizo 100,000 zimechangwa na wanachama katika mkutano huo.

Alisema wakati maandalizi ya kukabidhi fedha hizo ukiendelea siku hiyo ambayo SHIWATA imetenga kwa ajili ya kufanya kazi za kumuenzi baba wa Taifa, Nyerere viongozi wa kitaifa ambao walikuwa wapokee mchango huo watakuwa mkoa wa Simiyu katika sherehe ya kuzima Mwenge wa Uhuru.

Katika mkutano huo wanachama waliahidi kuendelea kuchangia matukio yote ya kijamii na wengi wameahidi kuwasilisha vifaa mbalimbali na nguo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera.

Wakati huo huo SHIWATA imetoa ofa ya Sh. Mil. 3.2 kwa wanachama wake watakaojenga nyumba za kuishi katika kijiji chao cha Mwanzega Mkuranga. Akifafanua kuhusu ofa hiyo, Taalib alisema gharama za kusafirisha vifaa vya ujenzi, gharama za kusafisha eneo la kujenga na ekari moja ya kulima bustani watapewa bure.

Alisema kasi ya wanachama kujenga na kuhamia kijijini inaridhisha mpaka sasa nyumba 200 zimekamilika na nyingine zinaendelea kujengwa. Taalib huduma za jamii kijijini hapo zinafanyiwa kazi ambapo huduma ya maji safi na salama ya kisima kirefu itapatikana mapema.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib akizungumza na wanachama wa mtandao huo wakati wa mkutano wa kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi, Kagera.Picha na Mpiga picha wetu. 
Mwanachama wa SHIWATA, Hamisi Kiondo akichangia hoja ya namna ya kusaidia waliopatwa na maafa Kagera. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...