MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)umeandaa mashindano ya Sanaa na Michezo litakalofanyika kuanzia Novemba 12,2016 katika viwanja
mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib alisema jana kuwa michezo
itakayoshindaniwa ni soka,mpira wa kikapu,ngoma za asili, muziki wa
dansi, sarakasi, Karate na kaswida.

Alisema mashindano hayo yatafanyika kuwapata washindi ambao kwa pamoja watakwenda kukabidhiwa zawadi zao kwenye kijiji cha wasanii
Mwanzega,Mkuranga.

Mwenyekiti Taalib aliwataja wajumbe wa Kamati ya tamasha hilo kuwa ni
Deo Kway, na mchezaji wa zamani wa Simba, Kureshi Ufunguo na mchezaji
wa zamani wa Yanga, Salvatory Edward watakaosimamia mashindano ya
soka.

Wengine ni Selemani Pembe, Athumani Bakari maarufu kama Mbegeja katika mchezo wa sarakasi,Abdul Salvador kamati ya muziki wa dansi na Kocha wa timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu, Manase Zablon katika mchezo wa mpira wa kikapu.

Wajumbe wengine ni Ismail Kambangwa, Kashindye Fundikira na Mariam
Ismail maarufu kama mama Mipango watakaosimamia ngoma za asili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...