Shule ya Atlas Madale iliyopo Jijini Dar es Salaam imefanya mahafali ya Darasa la saba, ambapo Mgeni rasmi kwenye mahafali hayo alikuwa ni ndugu Rogers Shemwelekwa, ambae ni Afisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni.

Mkuu wa Shule ya Atlas Madale Justus Kagya akizungumza katika Mahafali hayo ameeleza kuwa kila mwaka ifikapo Oktoba 14 shule hiyo imejiwekea utaratibu wa kufanya mahafali ili Kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu JULIUS NYERERE.

Makamu mkuu upande wa Taaluma kwenye shule hiyo Joseph Mjingo amewataka Wazazi kuacha kuwakatisha tamaa Watoto, hususani kwenye Somo la Hesabu, ambalo limekuwa likionekana kuwa ni gumu tofauti na masomo mengine

Aidha Mahafali hayo yamehudhuriwa na Wazazi pamoja na walezi wa wanafunzi hao.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakipata maelezo ya kina kutoka kwa mkuu wa Shule ya Atlas madale, ndugu Justus Kagya wakati wa mahafali ya wahitimu wa Darasa la saba kwenye shule, ambayo pia yalihudhuriwa na wazazi na walezi wa wanafunzi hao. 
Wazazi wa wanafunzi wanaohitimu elimu ya msingi katika Shule ya Atlas madale ya Jijini Da es Salaam wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kwenye Shughuli hiyo.
Sehemu ya Wanafunzi wa Atlas madale waliohudhuria Mahafali ya wahitimu wa Darasa la Saba kwenye Shule hiyo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...