Kila siku ya tarehe 15 Oktoba, Dunia nzima huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Umasikini, ambapo mwaka huu kauli mbiu ya siku hiyo ilikuwa ni

‘’KUTOKA UDHALILISHAJI NA UTENGWAJI MPAKA USHIRIKISHWAJI ‘’.

Mtandao wa Dini mbalimbali kwaajili ya watoto ulimwenguni uitwao Global Network of Religion for Children (GNRC-Tanzania) wamefanikiwa kuhitimisha siku hii kwa namna ya pekee kabisa ambapo tangu tarehe 15 Oktoba wamekuwa wakiandaa matukio mbalimbali yaliyolenga kuwajengea uwezo watoto haswa wa Shule za msingi kwa kuandaa mashindano tofautitofauti kama Midahalo na Michezo ikiwa na lengo la kuwajengea watoto uwezo (capacity building) na kuwapa elimu ambayo itaweza kuwakomboa katika janga la umasikini .
Wanafunzi wa shule ya Msingi Oysterbay wakiwa kwenye picha ya pamoja na Baraka Chedego kutoka GNRC -Tanzania kabla ya kuanza kwa mechi ya mpira wa miguu.
Mfano wa vyeti walivyotunukiwa wanafunzi kutoka na ushiriki mzuri wa siku hii ya kipekee.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...