HAKUNA mbabe, ule mtanange uliokuwa unasuburiwa kwa hamu kubwa uliohusisha mahasimu wawili Yanga na Simba umemalizika jioni ya leo kwa timu hizo kutoka sare ya 1-1.
Katika mchezo huo uliokuwa na presha kubwa kwa kila upande, Yanga walifanikiwa kupata goli dakika ya 26, baada ya Amisi Tambwe kumzidi mbinu beki Novat Lufungo wa Simba na kuandika goli la kuongoza huku nahodha Jonas Mkude akipewa kadi nyekundu baada ya kumpiga mwamuzi kwa kudai kuwa Tambwe aliushika mpira kwa mkono.
Mpira ulisimama kwa dakika takribani tano kutokana na  vurugu kutokea ikiwemo mashabiki wa Simba kuanza kung'oa viti na kuvirusha uwanjani, hali iliyopelekea Jeshi la Polisi kuanza kupiga mabomu ya machozi ili kutuliza ghasia iliyojitokeza uwanjani hapo.
 Mpaka ilipofika mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa goli 1-0, lakini kipindi cha pili Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa Kelvin Yondan aliyekuwa na kadi ya njano na kuingia Andrew Vicent "Dante", Saimon Msuva akachukua nafasi ya Juma Mahadhi, Haruna Niyonzima akiingia baada ya Deus Kaseke, Simba wakimtoa Laudit Mavugo na kuingia Fredrick Blagnon, Ibrahim Ajib na kuingia Mohamed Ibrahim na Novat Lufungo na kuingia Jurko Murshid.
Mchezo uliokuwa wa kasi kwa kila upande huku Yanga wakitafuta goli la kuongoza na Simba wakisaka la kusawazisha, ambapo dakika ya 89 Shiza Kichuya anawainua mashabiki wa Simba baada ya kupiga kona iliyoenda moja kwa moja wavuni na kusawazisha na kudumu mpaka dakika 90. Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 

Beki wa Yanga, Juma Abdul akimchezea rafu kiungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (Mchezo wa Watani wa Jadi), uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam leo. Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1. 
Mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya akishangia baada ya kuipatia timu yake goli la kusawazishi dhidi ya Watani wao wa Jadi, Yanga ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akiipatia timu yake goli, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
 Mabomu ya machozi yarindima jukwaa la mashabiki wa Simba ili kutuliza ghasia iliyojitokeza uwanjani hapo.
Mshabiki akipiga mateke viti vilivyong'olewa na kurushwa uwanjani 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. simba na yanga walipie gharama za kukarabati uwanja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...