SIMU.TV: Waziri mkuu amesema amefurahishwa na jumuiya ya kikristo Tanzania CCT na kanisa katoliki kwa kuamua kujenga makao makuu yake mkoani Dodoma. https://youtu.be/_4IJVGWqyBM

SIMU.TV: Hospitali ya rufaa ya Kitete mkoani Tabora inakabiliwa na uhaba wa vitanda na majengo ya wagonjwa hali inayowalazimu mama wajawazito kulala wawili hadi watatu. https://youtu.be/lYzPEYHmXEs

SIMU.TV: Baraza la taifa la uhifadhi wa mazingira NEMC limeitoza faini ya shilingi milioni 25 shule ya Al muntazir ya jijini Dar es Salaam kwa kutiririsha maji taka kwenda eneo la bahari. https://youtu.be/jUVgeN1JCgs

SIMU.TV: Ukosefu wa mabweni kwa shule za sekondari umetajwa kuwa changamoto inayosababisha vitendo viovu kama uvutaji wa bangi. kwa wanafunzi. https://youtu.be/_eiftjWtiL0

SIMU.TV: Kampuni ya mafuta ya Lake Oil imetoa jumla ya madawati 50 kwa shule ya msingi Kibugumo jijini Dar es Salaam  ikiwa ni kuunga mkono juhudi za kumaliza tatizo la madawati. https://youtu.be/QsiGDXH3FMs

SIMU.TV: Utafiti umeonesha kuwa ongezeko la watoto wa mitaani na wanaoishi kwenye mazingira magumu unasababishwa na migogoro katika familia pamoja na kipato duni. https://youtu.be/RLNrJp3u10Q

SIMU.TV: Kampuni ya bia ya TBL imelenga kupanua wigo wa kuuza bidhaa zake hapa nchini ili kuongeza mapato ya kampuni na ulipaji wa kodi. https://youtu.be/t_rxsJln168

SIMU.TV: Wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wamepewa siku kumi na nne kuondoka maeneo yote yasiyo rasmi na kwenda maeneo waliyopangiwa. https://youtu.be/5B0Re1b-KtI

SIMU.TV: Makampuni nchini yamekumbushwa kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kusaidia kuendeleza huduma za kijamii kama elimu na maji. https://youtu.be/OfpFqsDyYI0

SIMU.TV: Jumla ya timu kumi na mbili zinatarajia kushiriki katika ligi ya wanawake nchini inayoanza Novemba mosi mwaka huu na kuoneshwa moja kwa moja na vituo vya televisheni vya Azam. https://youtu.be/l7ZvdnPC79U

SIMU.TV: Timu nyingi zimeshindwa kushiriki katika mashindano ya netball yanayofanyika mkoani Ruvuma na kufanya timu tatu tuu kushiriki. https://youtu.be/UJfsmztBQrk

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...