THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

SINGELI MICHANO CONCERT KUFANYIKA OKTOBA 14 MBAGALA ZAKHIEM.

KWA mara ya kwanza katika historia ya Muziki Tanzania,  Efm Radio inakuletea mkazi wa jiji la Dar es salaam, Tamasha kubwa, litakalowakutanisha wasanii wa muziki wa Singeli Tanzania nzima  ambapo zaidi ya wanamuziki 100 wa singeli wataperfom katika jukwaa moja pale Dar live, Mbagala Zakhiem octoba 14, 2016. Kuanzia kumi kamili jioni hadi kuchee.

 Efm redio itahakikisha mashabiki wa muziki huo wa singeli wanaburudika pamoja na wanamuziki wa muziki huu wa singeli kutambulika Tanzania nzima.

Unaacha buku  tano tu mlangoni na kushuhudia wakali wote wa singeli Tanzania wakiperfom akiwepo Dogo Nigga, Sholo Mwamba, Dula Makabila, Msaga sumu, Eskide Virus, Majid Migoma, Mc Miduku, Maseke,  Kaja kaka Mpemba, Machupa, Msaga Lami, Segu Segumbo, Makaveli na wengine kibaoo.

Vilevile tamasha hili litaenda sanjari na semina kwa wasanii wote wa singeli hasa chipukizi ambapo watoa mada watakuwa ni kutoka BASATA, TCRA,TRA na Mgeni rasmi kwa ajili ya ufunguzi wa semina hiyo anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel Mollel.

Lengo ni  kuwafundisha maadili, jinsi ya kulipa kodi, na ni jinsi gani wataendeleza kazi zao kwa kujenga mahusiano mazuri na Taasisi hizo za Serikali.