Na Bashir Yakub.
Kurasimisha biashara kunazo namna nyingi. Kufungua kampuni ni moja ya namna ya kurasimisha biashara. Kusajili jina la biashara nayo ni namna nyingine ya kurasimisha biashara. Makala yatazungumzia hii ya pili ya kusajili jina la biashara. Na hii ni kwasababu hii ni njia nyepesi, ya haraka, na ya gharama ndogo sana.
Mfano wa jina la biashara ni kama, HK bazaar, kinondoni investment, Congo traders, Karoli LTD na mengine yanayofanana na hayo.
1.NINI MAANA YA JINA LA BIASHARA.
Jina la biashara ni lile jina linalotumiwa na mtu kama jina la utambulisho wa biashara yake inayofanywa katika mfumo ambao sio kampuni. Makampuni yana majina lakini majina hayo hayawezi kuitwa majina ya biashara bali ni majina ya kampuni.
Jina la biashara ni kwa yule ambaye biashara yake imesajiliwa lakini sio kampuni.
Aidha mwenye biashara ambayo haijasajiliwa lakini analo jina fulani analotumia kisheria huyo hana jina la biashara.Hilo jina sio lake na mtu mwingine anaweza kulisajili na akamtaka huyu ambaye hajalisajili kuacha mara moja kulitumia .
Ili sheria ikutambue kuwa una jina la biashara ni pale tu unapokuwa umesajili jina hilo.
2. WAPI WAWEZA KUSAJILI JINA LA BIASHARA.
Jina la biashara husajiliwa kwa msajili wa biashara na makampuni ( BRELA). Ukifika hapo utawaeleza kuwa unataka kusajili jina la biashara watakupa fomu maalum utaijaza . Lakini kabla ya hapo utatakiwa utume maombi maalum hapohapo BRELA ukitaka kujua iwapo jina ulilochagua kuwa la biashara yupo mtu mwingine analitumia au lah.
Hii ni kwasababu jina ni moja Tanzania nzima. Hakuwezi kuwa na majina mawili au zaidi yanayofanana huku yote yakiwa yamesajiliwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...