THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TAARIFA KWA WANAJUMUIYA NA MARAFIKI JUU YA MISAADA ITOAYO TCO

 
TANZANIA COMMUNITY ORGANIZATION  
OF NORTHEN CALIFORNIA (TCO)  
912 Bayview Ave, Oakland, CA 94610  
510.290.9708, 510.472.7672 

Ndugu Watanzania na marafiki wa Northern California. 
Mwaka huu tutakuwa na fundraising nyingine ambayo itaambatana na kusheherekea kumbukumbu ya sherehe zetu za uhuru hapo Dec 10 2016.  Fundraising ya mwaka huu itakuwa ni kusaidia  vifaa/kifaa kwa zahanati (clinic) mojawapo kutoka kijiji kimojawapo Tanzania. 
Lakini kabla ya yote ni vizuri tuwape taarifa kwa ufupi juu ya juhudi zenu mlizofanya mwaka jana za kuwezesha kuchangia msaada wa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi (albino)

Shughuli ilifanyika Dec 19 2015 katika mji wa Oakland - CaliforniaKatika mapato yaliyopatiakana basi Umoja wetu (TCO) uliweza kusaidia shule ya msingi ya Buhangija ambayo ni shule ya albinos  inayosaidia kuwasomomesha watoto hawa katika mazingira ya amani baada ya matukio ya kukatwa viungo kuwa mengi miaka michache iliyopita. 
TCO (Tanzania Community Organization) kupitia michango yenu iliweza kusaidia kiasi cha milioni 6, tisini na saba elfu (tsh 6,097,000)
Kiasi hiki kilitumwa kupitia kwenye serikali ya wilaya kwa kushirikiana na uongozi wa shule ili kuhakikisha msaada uliwafikia walengwa.Matumizi yake yalikuwa kama ifuatavyoWanafunzi waliweza kusaidiwa : 
1.Mashuka 200 kwa gharama ya tsh milioni mbili (2,000,000 tsh) 
2. Kofia kubwa (kwa ajili ya jua) na tshirts 200 kwa gharama ya milioni moja na laki sita (1,600,000 tsh) 
3. Vyandarua 100 kwa gharama ya laki nane (800,000 tsh) 
4.Sweta 200 kwa gharama ya milioni moja laki sita na tisini na saba (1,697,000 tsh) 
Tunaomba wadau wote na watanzania kwa ujumla kwenye jumuiya yetu tuendelee kuwa mstari wa mbele katika kusaidia misaada mbalimbali katika jamii mbalimbali zenye mahitaji huko Tanzania. 
TCO itaendelea kuwa mstari wa mbele kila mwaka kuendeleza zoezi hiliKwa pamoja tutainuana. 
Karibu na changia kwa bidii tarehe 10 Dec 2016 Oakland- California kwenye hii. 
Tembelea website yetu 
Erick Byorwango 
(Mwenyekiti- Uhusiano na Uenezi TCO)