Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa yeyote anayetaka kuwa Mdadisi au Mkusanyaji taarifa za kitakwimu rasmi katika tafiti mbalimbali zinazoratibiwa na ofisi hii, ni sharti awe amehitimu Mafunzo ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi angalau kwa ngazi ya cheti.

Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu Na. 9 ya mwaka 2015 inayoipa mamlaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya kuratibu na kusimamia ukusanyaji takwimu rasmi (official statistics) nchini. 

Hivyo, kuanzia sasa NBS itakuwa inawatumia wadadisi ambao wamehudhuria na kuhitimu angalau cheti cha Ukusanyaji Takwimu katika miradi mbalimbali ili kuboresha zaidi upatikanaji wa takwimu rasmi nchini.

Mafunzo ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi yanatolewa na Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika “Eastern Africa Statistical Training Centre” (EASTC) kilichopo Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
Kwa mawasiliano zaidi na kujisajili wasiliana na:

Ofisi ya Msajili wa Chuo,
Eastern Africa Statistical Training Centre,
S.L.P 35103,
DAR ES SALAAM.
Barua pepe: info@eastc.ac.tz; 
Tovuti: www.eastc.ac.tz  
Simu namba: 022-2925000 au 0784784106.

Tangazo hili limetolewa na:    
Mkurugenzi Mkuu,
Ofisi ya Taifa ya Takwimu,
DAR ES SALAAM.
05 Oktoba, 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...