Kamati ya maafa mkoani Kagera imeendelea kupokea misaada kutoka kwa wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kutoa michango yao kwa lengo la kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililoathiri mkoa wa Kagera.

Akikabidhi msaada uliotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini Mwanza Mratibu Mkuu wa taasisi hiyo Bw. Burhan Mohammed amesema kuwa wao kama taasisi wamevutwa na kushikwa kwa moyo wa huruma na kuamua kuchukua hatua ya kuwasidia majirani zao wa mkoa wa Kagera. "Sisi sote ni Watanzania, tuliposikia wenzetu wamepatwa na matatizo, tumeamua kutoa mchango wetu kwa kushirikiana na wanachama wenzetu ili kutoa huduma za kuwapa chakula wenzetu wakati wa matatizo" alisema.

Taasisi hiyo imetoa Mchele, chumvi, mafuta ya kula, Sabuni pamoja na katoni za maji ya kunywa ambapo vyote kwa jumla vinathamani ya sh. milioni 22. Aidha, Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Lwelu ya mkoani Kagera wametoa vyakula vyenye thamani ya shilingi milioni 2.1 ikiwa ni pamoja na sukari, unga na mchele.

Wadau wengine waliotoa misaada ni kampuni ya Time to Help yenye makao makuu ya jijini Dar es salama ambayo inayomilikiwa Waturuki wametoa mablanket 500. Akipokea misaada hiyo kwa niaba ya Mkuu Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro amewaeleza wadau hao taswira mzima ya hali ya maafa katika mkoa Kagera ambapo amesema kuwa mahitaji kwa waathirika bado ni makubwa.

Kwa niaba ya Serikali, Mkuu wa Wilaya Bw. Kinawiro amewashukuru wadau wote wanaendelea kutoa misaada kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa Kagera ambao wameathirika wa tetemeko hilo na kuwataka wadau wengine kuendelea michango ya hali na mali katika kukabiliana na hali ya maisha baada ya tetemeko kutokea.
Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro akiwashukuru Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini Mwanza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu na kusema kuwa mahitaji kwa waathirika wa tetemeko la ardhi bado ni makubwa na misaada inahitajika ili kuwasaida waathirika hao.

Mratibu Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini Mwanza Burhan Mohammed akitoa neno mwishoni mwa wiki mara baada ya ya kukabidhi msaada wa vyakula kuwasaidia wakazi wa mkoa wa Kagera ambao wameathiriwa na tetemeko la ardhi mapema mwezi Septemba mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawiro (katikati aliyevaa suti) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Taasisi ya Kimataifa ya Lions Club ya jijini Mwanza mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula kuwasaidia wakazi wa mkoa wa Kagera ambao wameathiriwa na tetemeko la ardhi mapema mwezi Septemba mwaka huu. (Picha/Habari na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba). 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...