OKTOBA 11 ya kila mwaka, dunia huadhimisha siku ya wasichana duniani. Katika kuelekea siku hiyo, Taasisi ya Doris Mollel chini ya Mkurugenzi wa Idara ya Elimu, Rahma Amood ilipokea vitabu vya kiada zaidi ya 200 kutoka kampuni ya MAK SOLUTIONS.

Kampuni ya MAK SOLUTIONS inayohusika na uuzaji na usambazaji wa vitabu, ilitoa vitabu hivyo ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Taasisi hiyo yenye lengo la kusaidia shule zenye uhaba wa vitabu hususani za wasichana zinazopatikana katika mikoa ya Arusha, Pwani, Dar es Salaam na visiwani Zanzibar

Akizungumza wakati wa kupokea vitabu hivyo, Rahma Amood alisema alisema kuwa “ vitabu ni muhimu sana kwa mwanafunzi kwa sababu vinaongeza uelewa wa kile kinachofundishwa darasani, sisi kama Taasisi ya Doris Mollel tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya MAK SOLUTIONS kwa kuunga mkono jitihada zetu” alisema.

Kwa upande wa MAK SOLUTIONS kupitia kwa Mkurugenzi wake, MEETAL KIRUBAKARAN alisema “tutaendelea kushirikiana na Taasisi ya Doris Mollel kwa sababu wameonesha nia ya kusaidia wasichana ili waweze kupata elimu bora, hivyo basi kwa kupitia wao tutaweza kuwawezesha wasichana wengi katika jamii yetu”.
Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel hapa nchini, Bi. Doris Mollel (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Watendaji wa kampuni ya MAK SOLUTIONS mara baada ya kupokea vitabu vya kiada zaidi ya 200 kwa ajili wa shule zenye uhaba wake. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Elimu wa Taasisi hiyo, Rahma Amood.
Sehemu ya vitabu hivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...