Na Dotto Mwaibale

VIJANA wasomi wametakiwa kuacha kutegemea kazi za kuajiriwa badala yake wawe wabunifu katika masuala mbalimbali kulingana na elimu yao ili kujikomboa kiuchumi.

Mwito huo umetoewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lecri Consult, Edna Kamaleki Dar es Salaam leo katika warsha ya siku mbili ya kuwaongezea uwezo vijana iliyoandaliwa na taasisi hiyo. 

"Kijana umesoma kwanini upoteze muda wako kwa kuzunguka kutafuta kazi wakati fursa nyingi zipo" alisema Kamaleki.Kamaleki aliwataka vijana waoshiriki warsha hiyo kubadili na kuthubutu kuanza kufanya kitu chochote kulingana na elimu walizosomea vijana hao.

Akizungumzia taasisi yake hiyo alisema imejikita kutoa huduma za kisheria kwa jamii na ushauri katika mambo mbalimbali yanayohusu haki za watoto."Tuna amani kwamba haki za watoto ni muhimu kwa maendeleo na ustawi wa watoto, pia watoto wanapaswa kuishi katika jamii ambayo haki za binadamu na sheria zinaeleweka vizuri na kuheshimiwa na kila raia" alisema Kamaleki.

Alisema taasisi hiyo inatoa ushauri na huduma ya kisheria kwa jamii wakiwemo watoto, watu binafsi na taasisi mbalimbali na kuandaa nyaraka mbalimbali za kisheria na mikataba ya kisheria.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lecri Consult, Legal and Child Right Consult, Edna Kamaleki (kushoto), akizungumza na vijana wasomi katika warsha ya siku moja ya kuwaongezea uwezo iliyofanyika Dar es Salaam leo. Warsha hiyo iliandaliwa na taasisi hiyo.
Mdau Julius Kionambali (kushoto), akizungumza katika warsha hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...