TAASISI isiyo ya kiserikali ya Mathayo Suleiman Foundation yatoa msaada wa vyakula katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman, amesema kidogo walicho nacho kinaweza kuwasogeza siku mbili tatu watoto wanaoishi katika kituo hicho kwani kinakabiliwa na uhaba wa chakula kwa kiasi kikubwa sana.

Pia amesema kuwa katika maisha tumetofautiana ndio maana wanachama wa taasisi hiyo wameona watoe kile kidogo walichokuwa nacho kwani kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake.

Nae Mratibu wa Kituo  cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam, Isa Buzohera amewashukuru wanachama wa Taasisi hiyo kwa kutoa mchango wao kwani taasisi ilikuwa katika hali mbaya sana ya ukosefu wa chakula.

Amesema kuwa kituo hicho  Dogodogo Maltiporpuse Training Centre  mpaka sasa kinawatoto 39 wasichana 10 na wavulana 29 amesema kituo hicho Kilifunguliwa 2003 kwa lengo la kuwapika kiufundi watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze kujitegemea wakiwa na nyenzo mhimu ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Amesema kuwa uhaba wa chakula ukiendelea kituo hicho kitafungwa kwani mpaka sasa wanahitaji zaidi ya Milioni 205 kwaajili ya chakula pamoja na vifaa vya kuwapa kila mhitimu wa mafunzo yanayotolewa katika kituo hicho. 
Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman (Mwenye suti nyeusi katikati) akikabidhi mbuzi kwaajili ya nyama kwa Mwalimu wa kituo cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam, Rosemary Nyabuzuki leo. Wengine ni wanachama wa Taasisi ya Mathayo Suleiman.
 Mratibu wa Taasisi ya Mathayo Suleiman, Banga Suleiman(Mwenye Suluali Nyeupe) akishirikiana na wanachama wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation wakikabidhi unga kwa watoto wa kituo cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam leo.
 Wanachama wa Taasisi ya Mathayo Suleiman wakimsikiliza Mratibu wa Kituo cha Dogodogo Maltiporpuse Training Centre kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam, Isa Buzohera katika kituo hicho leo.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaph Suleiman akizungumza mara baada ya kupata maelezo ya kituo cha Dogodogo Multiporpuse Training Centre.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...